Programme Américain d’Admission des Réfugiés

Kipindi cha 3: Kipimo cha Matunzo

 

 

 

Kipindi cha 3: Kipimo cha Matunzo

 • Kusikiya - Kipindi cha 3: Kipimo cha Matunzo
  Kusikiya

Ikiwa kesi yako ina endeleya, wewe na kila mwana memba wa familiafamilia kwa kesi yako, muta pangwa kwa kipimo cha matunzo ambayo ina lazimishwa. Uje na vikartasi vyote vya matunzo naza nduwi ulizo kuwa nazo kwenye mkutano. Iyi itakuwa muhimu sana kwaku chukuwa muelekeo unao faa kwa mambo ya matunzo na afya katika mwendo wa kuhamishwa (réinstallation) na baada kufika kwako Marekani. Uhalali wa Uchunguzi wa kimatibabu ni kati ya myezi 3 hadi 6. Una weza kupimwa upiya ikiwa hau kusafiri umarikani kabla tarehe ya uchunguzi wa kimatibabu haujamalizika.

Uchunguzi wa kimatibabu vina lenga ku hakikisha yakuwa una jibu kwa shurti za afya kwaku ingiya Marekani, una weza safiri, kupata musaada wa matunzo unao stahili ku fwatana na haja na hauoneshe hatari kwa wengine wasafiri.

Kipimo ca Matunzo inakuwa ni haya:

 • Macunguzi ya hali ya muhimu wa afya ya umma
  Ugunduzi wa shurti za afya zinazo omba maelekezo zaidi
  Utambulisho wa hali za afya zinazo omba mpangilio zaidi kabla ya kuondoka, kusafiri, na baada ya kufika na kuwahamishwaUsawa kwa utambulisho za kusafiri, matibabu, na kusindikizwa kwa matibabu, wakati inahitaji.

*Watu walio na hali mbaya za afya watapewa kuzindikizwa kwa matibabu kwaku saidiya wakati wa safari yao kwenda Marekani

SWALI ZINAZO ULIZWA MARA NYINGI

Je! Ni tegemeye nini wakati wa uchunguzi wa kimatibabu

Kwa kipimo chako na kulingana na mwiaka yako unaweza ku pimwa:

 • Shinikizo la damo, urefi, unene, na vipimo vya maco
  Vipimo bya damu
  Nakufanya picha ya kifuwa
  Vipimo vya mwili ambayo vina fanika
  Ma chango (Immunizations) zilizo tolewa

Je! Ni tegemeye nini baada ya uchunguzi wa kimatibabu?

Unapomaliza uchunguzi wako wa matibabu, inaweza kuchukua wiki kadhaa kabla ya matokeyo kukamilika na kushirikiwa na Kituo cha Msaada wa kuhamisha (centre de support pour la reinstallation).Kufata na iyi mwendo unaweza pengine kupata vipimo vingine.Ikiwa ndio kesi, unaweza kuitwa na daktari au wafanyikazi wa RSC ili kupanga miadi ya kufuata.Fomu za uchunguzi wa matibabu zina kipindi cha uhalali wa miezi 3 hadi 6 baada ya uchunguzi wa mwili na, kulingana na michakato mingine ya kuhamishwa( reinstallation) na ukaguzi unatakiwa pengine kupata uchunguzi wa afya kwa mara ingine.

⇠ Kila Kitu kuhusu USRAP