Programme Américain d’Admission des Réfugiés

Kiingiliyo

 

 

 

Mpango wa uhamiaji wa wakimbizi wa Marekani

 • Soma - Mpango wa uhamiaji wa wakimbizi wa Marekani
  Soma
 • Kuona - Mpango wa uhamiaji wa wakimbizi wa Marekani
  Kuona

Maelezo ya Jumla ya USRAP

 • Kusikiya - Maelezo ya Jumla ya USRAP
  Kusikiya

Mapitio ya Mpangilio wa Programme ya Réception na Placement (R&P) ya Marekani

 • Kusikiya - Mapitio ya Mpangilio wa Programme ya Réception na Placement (R&P) ya Marekani
  Kusikiya
 • Kuona - Mapitio ya Mpangilio wa Programme ya Réception na Placement (R&P) ya Marekani
  Kuona
 • Soma - Mapitio ya Mpangilio wa Programme ya Réception na Placement (R&P) ya Marekani
  Soma

Ukiwa wewe ni mukimbizi na hauwezi ku rudi kwa inchi yako ya asili. Unaweza ruhisiwa kuhamishwa yakudumu kwa inchi nyingine. Niiyo wana ita réinstallation.

Kwa kuhamishwa upya katika inchi nyingine, una takiwa kuitikiwa katika mwendo yaku andikwa kawaida. Inchi zote zinazo itika wakimbizi kwa kuwashimika upya wanakuwa na mwendo za hamisho upya (réinstallation ) tafauti

Nchi ya Marekani ni kati ya inchi duniyani zinazo itika wakimbizi kwajili ya ku wahamisha upiya. Toka mwaka wa 1980, wa Amerika wamesha pokeya wakimbizi zaidi ya milioni 3 toka duniya nzima kupitiya Programme Américain d’Admission des Réfugiés, ao USRAP. Ili kuchukuliwa na USRAP, lazima uelekezwe na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ao kustahiki kuomba kupitia mojawapo ya Direct Access Programs.

Rasilimali na habari zinazotolewa hapa zinaelezea mchakato wa USRAP.

Mara tu unapoanza mfuatano ya mambo wa USRAP, hizi ni vipindi utakayopitia:

Kipindi cha 1: Interview ya uchunguzi
Kipindi cha 2: Interview ya USCIS
Kipindi cha 3: Uchunguzi wa kimatibabu
Kipindi cha 4: Orientation Culturelle
Kipindi cha 5: Safari
Kipindi cha 6: Kufika

Kila kesi ya réinstallation ni ya kipekee na muda unaohitajika kukamilisha mfuatano ya mambo wa USRAP inategemea hali ya kila kesi.

Réinstallation ni chaguo inayo patikana tu kwa wakimbizi wachache tu na kumaliza mwendo itaomba wakati na bidii toka kwako piya kwa serkali ya Marekani. Kabla yaku anza mwendo unatakiwa ku hakikisha kuwa tayari kuhamishwa Marekani ikiwa una kubaliwa. Kazi zote za mahamisho (réinstallation) ni bure. Akuna wakati katika mwendo mtu anaweza kuku omba pesa kwajili ya kazi ya réinstallation. Mtu akiku omba pesa, anaku kulazimisha uombe, ao anaonesha kuwa ana weza saidiya ku harakisha ombi lako au kuku tidha kwa namna yeyote tafazali uijulishe. Utapewa maelezo kuhusu namna yaku julisha udanganyifu kwa interview yako ya kwanza. Kila Centre de Support pour la Réinstallation iko na email addresse ya ku ripoti udanganyifu.

(Centre d’Appui à la Réinstallation = RSC)

⇠ Kila Kitu kuhusu USRAP