Kwa wakati fulani kabla yakuondoka kwako kwenda Marekani, Centre de Support pour la Réinstallation itaku alika piya kuhuzuriya kwa maelekeo ya kitamadumi (Orientation Culturelle) ambako mutapewa maelezo muhimu kuhusu safari yako Marekani na kwayale unategemeya utakapo fika.
Maelekeo ya kitamadumi (Orientation Culturelle) utakuanda kwa kuhamishwa (réinstallation) nakukupatiya maelezo kuhusu mila na ma sheriya za Marekani. Maelekeo ya Kitamaduni (orientation culturelle) itakusaidia kukuza matarajio ya kweli na ujifunze ujuzi na mitazamo inayohitajika kufanikiwa katika mazingira yako mapya. USRAP ime tiya mupango wa Mafunzo ya Orientation Culturelle inao tokona na myaka za zowezi. Mafunzo ya Orientation Culturelle inatolewa na mufanya kazi anaesema lugha mingi na anae juwa kabila nyingi atakaye wasaidiya kukunduwa tatizo za réinstallation kabla azija tokeya na kujibu kwa maswali zinazo ulizwa mara nyingi kuhusu réinstallation Marekani.
SWALI ZINAZO ULIZWA KILA MARA
Je! Ni kwa nini na weza tegemeya kwa wakati wa Mafunzo ya maelekeo ya kitamudumi (Orientation Culturelle)
Mafunzo ya maelekeo ya kitamudumi (Orientation Culturelle) ni mikutano ya majifunzo yana kuwa na lengo yaku kusaidiya ku zoweya kwa maisha yako mapya Marekani. Somo ni hizi:
- Kazi ya Agence de Réinstallation
Kazi
Nyumba
Elimu
Afya
Hudma za Jamii
Haki na Mapashwa
Kujifunza Kingereza
Usimamizi wa pesa
Uchukuzi
Marekebisho ya kitamaduni (Adaptation culturelle)
Je! Ikiwa siwezi kuhudhuria mafunzo ya Mila ya Kitamaduni (orientation culturelle)?
Ili upate ku faidiya ifahavyo, darasa za Orientation Culturelle zime undwa kwajili ya kuhuzuriya na ku jadiliyana. Tunawahimiza sana wana familia wote wanao stahili kuhudhuria.
Pengine haiwezekani ku huzuriya kwa darasa za Orientation Culturelle. Katika hali hiyo, utapokeya vikartasi vilivyo andikwa kwakuku saidiya kuji andaa kwa maisha Marekani. Tunakuunga mkono ku chunguza vikartasi hivyo vyote kabla yakuenda kwako. Utapokeya maelekeo ya kitamadumi (Orientation Culturelle) ya zaidi Marekani.