Orientation Culturelle Maono ya Pamoja

Elimu

Marekani, elimu ina patikana kwa watoto wote, bila kushikamana na uwezo wao, jinsiya, miaka, rangi, dini, mielekezo ya jinsiya, ama nganzi ya kijamii.

Elimu nchini Marekani

 • Soma - Elimu Umarekani
  Soma
 • Kusikiya - Elimu Umarekani
  Kusikiya
 • Kuona - Elimu Umarekani
  Kuona

Kusaidiya mtoto wako ndani ya masomo

 • Kuona - Kusaidiya Mtoto Wako Ndani Ya Masomo
  Kuona

Wakimbizi kujuwa Teknolojia Numerali (Technologie Numérique)

 • Soma - Wakimbizi kujuwa Teknolojia Numerali (Technologie Numérique)
  Soma
 • Kusikiya - Wakimbizi kujuwa Teknolojia Numerali (Technologie Numérique)
  Kusikiya

Shule za uma ni bure, na kuna kuwa sheriya na kanuni kuhusu elimu ya uma. Elimu ina lazimishwa kwa watoto wa miaka fulani tokeya utoto hadi miaka ya ujana. Miaka kamili kuhusu shurti ya elimu ina pangwa nakila jimbo. Shule zina tegemeya kuona wazazi wana jihusisha na elimu ya watoto wao kwa kuakikisha yakuwa wana fata majifunzo na kuwa saidiya kwa namna mbalimbali.

Watoto na Vijana

Shule za uma zinapatikana kwa inchi pote bila malipo. Kufatana na sheriya, shule za uma haziwezi kuchukuwa mwelekeyo wa dini fulani. Shule za kibinafsi zina patikana eneyo fulani fulani zimoja zinakuwa na mwelekeyo wa kidini. Shule za kibinafsi zinalipisha pesa ya mafunzo, ambayo inaweza kuwa ya bei kali.

Katika shule za uma, vijana wanaume na wabinti wana kuwa wote kwa darasa moja.

Shule ya chekecea (école maternelle). Kiwango hiki nikwa watoto kutoka miaka 3 hadi 5. Hai lazimishwe na sheriya na kawaida sio kwa bure.

Shule ya msingi. Kiwango hii kuanza na darasa ya chekecea (umri wa miaka 5) na ku endelea hadi darasa la tano au la sita (umri wa miaka 12).

Shule ya sekondari. Kiwango hii kwa kawaida ina 3jumulisha darasa la sita au la saba hadi darasa la nane au la kenda, kwa watoto wa miaka 12 hadi 14.

Shule ya sekondari. Kiwango hii kwa kawaida ina jumulisha darasa la tisa au la kumi hadi darasa la kumi na mbili, kwa watoto wa miaka 14 hadi 18. Wanafunzi wanao maliza kwa kiwango hii wana pewa cheti ya kisegondari.

Wanafunzi wanaokuwa na cheti ya shule ya kisegondari alama bora wanaendelesha elimu kwa chuo kikuu, lakini elimu ya juu sii bure. Mafunzo ya kiufundi kisha shule yakisegondari ya patikana pia na ni ya bei rahisi kuliko vyuo vikuu na yuniversiti.

Watu Wazima

 

Wa Amerika wanaamini yakuwa mtu hawezi kuwa mzee sana au kijana sana ili kujifunza mambo mapya. Majifunzo ya watu wazima na vijana inawezekana, lakini wakimbizi wangeli pashwa kwangaliya faida na hasara zaku anza majifunzo kuliko kutafuta kazi. Elimu inaweza kuongoza kwa bahati yaku pata kazi nzuri kwa ujiyo, lakini wakimbizi wanapaswa kutumika punde ili kujibu kwa haja zao wenyewe naza familia zao, na majifunzo ya watu wazima Marekani inaweza kuwa ya bei kali. Kwa wakimbizi wengi, chaguo bora inaweza kuwa kutumika muda wote na kwenda shuleni nusu muda.

Jamii nyingi zinatoa aina nyingi za fursa za elimu ya watu wazima kama vile:

 • Majifunzo ya Kingereza na kujuwa kusoma na kuandika.
  Majifunzo ya zaidi kwa mambo ya kitekinolojya ya kompyuta, luga za kigeni, na ujuzi za katibu.
  Developpement d’éducation Générale (GED) kwa watu wazima ambao hawana cheti ya shule ya kisegondari.
  Masomo za kukufundisha kazi (École Téchnique Vocationnelle)
  Vyuo (Colège communautaire [kikawaida mipango ya miaka 2])
  Vyuo ama yuniversiti (kikawaida mipango ya miaka 4).
  Mhitimu ambazo zina towa vyeti kwa widara nyingi.

Bei ya izo darasa, shule, na vyo vikuu zina pishana zaidi. Shule nyingi na vyo vikuu zina towa msaada wa kipesa kwa wana funzi wanao kuwa nao aja.

Urekebishaji wa kitamaduni

Shule za ki Marekani zina kuwa kwa jumla na mazingira ya darasa yaku wasiliyana tafauti na namna ya mafunzo ya hotuba na usemi zinazo tumikishwa kwa inchi zingine. Kunakuwa piya samani inaotolewa kwa wazo lipya na kazi ya kibinafsi. Kazi za pamoja ni muhimu lakini wana funzi wana pimwa kufatana na kazi wanazo zifanya wenyewe.

Wazazi wanaweza saidiya watoto wao kwa namna nyingi ata awajuwi vizuri Kingereza. Ona namna gani muzazi mukimbizi anaweza saidiya kwa elimu ya watoto wao:

 • Tafuta shule ina towa matembezi ya elimu ama muelekezo umetolewa kabla masomo ku anza.
 • Uliza mtoto aliyo funzwa siku ile.
 • Uliza mtoto yale anatakiya kufanya nyumbani ama chunguza kitabu cake ca kazi za nyumbani.
 • Uzuriya kwa mafunzo za Kingereza kama lugha ya pili ya masomo, ikiwa wana itowa, kwenye shule ya mtoto wako.
 • Uzuriya kwa mkutano ya wazazi na walimu.
 • Saidiya kwa shuguli zingine za shule kama vile timu ya michezo ya shule, ao kundi ya sanaa.
 • Saidiya ndani ya darasa ya mtoto wako.
 • Shindikiza mtoto wako ndani ya basi ama kwenye shule.
 • Saidiya mtoto wako kwa kazi zake za nyumbani.
⇠ Kila kitu kuhusu kufundishwa tabiya za Inchi (Orientation Culturelle)