Orientation Culturelle Maono ya Pamoja

Kurekebisha Mila

Kurekebisha mila ni mwendo unaochukuwa muda mrefu. Mwendo huu ni tafauti kwa watu tofauti, lakini kuna hatua fulani katika huu mwendo ambazo watu wengi wana pitiya kwa Kurekebishwa kwa mila mpya.

Kama wale wengine walioacha nyumba zao na kuhamishwa kwa nchi ya kigeni, pengine utahisi wasiwasi na hasira unapojaribu kuzoweya nchi yako mpya. Hisia hizi ni za kawaida na zina kuwa kwa muda. Unaweza hitaji miaka 2-5 ili uzoweye kabisa maisha ya jamii mpya. Kuzoweya yako itakuwa ya rahisi ikiwa utashirikiana na wale ambao wanakusaidia. Kuwa mtulivu, kuwa wazi na kujifunza njia nzuri za kushindana na shida na vikwazo vya mila inaweza kukusaidia kupunguza mwendo huu. Kupata kazi na kujifunza Kiingereza itakusaidia pia kuzoweya. Kujifunza kuishi katika mila mpya si rahisi, lakini inaweza kuwa pia zowezi nzuri wakati unajifunza mambo mapya na kupata ujuzi mpya.

U-Mchirizo wa marekebisho ya mila

Kuna vipindi ine za kawaida za marekebisho ya mila ambazo unaweza kuta katika mwendo wako wa marekebisho: muda wa furaha, kugongana kwa mila, marekebisho, na ujuzi.

Kipindi cha furaha

Unakuwa na hisiya za msisimko na furaha, kila kitu ni kipya na cha kusisimua na ni kizuri. Iyi ina tokeya mara nyingi kisha ya kuwasili mahali mpya.

Kipindi cha kugongana kwa mila

Unakuwa na hisia za wasiwasi na kuchanganyikiwa kama vile mgeni, jaribu kufanya kazi mahali ambapo ni tofauti na usipo pazoweya.

Kipindi cha marekebisho

Hisia zako zina punguka wakati una toka kwa kipindi cha kugongana kwa mila na kuanza kujisikia vizuri zaidi na mjasiri katika shirika lako mpya.

Kipindi cha ujuzi

Unakuwa na hisia ya faraja na maisha yako mapya na mila, ingawa bado pangale wakati ngumu.

Njia za kukabiliana na mgogangano wa mila zinaweza husisha kushirikiana na marafiki, kucheza michezo au kuwasiliana na vipato vya dini na vya kiroho. Ikiwa wewe au mwanameba wa familia yako anahisi kuwa hawezi kukabiliana na matatizo ya maisha yako mapya Marekani, tafuta msaada mara moja.

Kujihusisha na jamii za mahali kwa kuhuzuria matukio yaki mila au kujitolea pia kunaweza kusaidia kupunguza kuzoweya kwako maisha ya Marekani. Kushiriki kwa jamii ni njia ya kukutana na washiriki wengine wa kikundi chako cha kidini, lakini pia kukutana na Waamerika na kufanya mazoezi ya Kingereza. Wafanyakazi wa ushimikaji watakusaidia kujifunza mengi kuhusu shirika yako mpya. Chunguza jamii yako mwenyewe pia.

Nguvu ya familia

Uhamishaji unaweza tuma nguvu ya familia kwa kubadilisha majukumu yaliyopo. Mabadiliko katika majukumu ya familia ni moja katika sehemu zenye kusumbua uhamishaji ya wakimbizi. Hata hivyo, kuna njia nzuri za kukabiliana na mabadiliko haya ya majukumu. Kuwasiliana waziwazi na kwa uaminifu na wato wa familia ili kila mtu awe na wazo nzuri la kile kila mtu katika familia anahisi na anachopitia.

Wazazi wa wakimbizi wanaweza kabiliana na changamoto wakati watoto wao wanapo zoweya mila mpya kwa haraka na tofauti kuliko wao. Wazazi hawapendi mambo ambayo watoto wao wanataka kufanya au njia nyingi wanazo zi zungumza na kutenda. Lakini zowezi fulani za uzazi zinaweza kuwa hazikubaliki au hata kinyume ya sheria Marekani. Ikiwa una wasiwasi juu ya familia yako au unajitahidi na watoto wako, wasiliana na mtu katika Agence de Réinstallation. Wanaweza kukusaidia au kukuunganisha na huduma za familia au mpango katika shirika lako.

Maadili ya Marekani na kanuni zaki mila

Marekani ziko na jamii tofauti, zina undwa na watu wa jamii tofauti, ukabila, maoni ya kidini na zowezi nyingine au imani, bado kuna kanuni na matarajio ya kimila ambayo yanaenea kabisa Marekani. Kuonyesha uvumilivu na heshima kwa watu wote bila ingawa imani na asili zao ni thamani muhimu kwa Waamerika wengi. Unatakiwa kuwa na uvumilivu na heshima kwa wale walio tofauti na wewe na unapaswa kutarajia uvumilivu sawa na heshima kutoka kwa wengine.

Matendo zako fulani yaki mila yanaweza kutofautiana na ya Waamerika wengi. Zowezi nyingine zinaweza kuchukuliwa kuwa hayakubaliki na pengine kinyume na sheriya. Ingawa Waamerika wana uwazi kwa mila zao na njia za kufanya mambo, kuna maadili fulani ya msingi, imani na zowezi ambazo wanatarajia wakazi wa Marekani kufuata.

  • Filosofiya ya kuji tosheleza ki binafsi na utetezi wa kibinafsi ni muhimu kwa mila ya Marekani na kurekebisha mila.
    Wamarekani wanaamini usawa wa jinsia na wanasamini uhuru wa wanaume na wanawake.
    Watu wanatarajiwa kufika kwa wakati kwa ajili ya mpango waku kutanana na mikutano, ikiwa ni ya utaalamu au binafsi. Kuchelewa inaonekana kama kukosa heshima na kwa wakati mwingine kuchelewa kunaweza kuwa na matokeyo makubwa. Unaweza kupoteza kazi yako ikiwa unachelewa kufika kazini, na unaweza kupoteza mpango waku kutanana wako ikiwa hautakutana na mfanyakazi wako wa kesi kwa wakati, daktari au watoa huduma wengine.
⇠ Kila kitu kuhusu kufundishwa tabiya za Inchi (Orientation Culturelle)