Orientation Culturelle Maono ya Pamoja

Huduma za Jamii

Huduma za mahali unakaa (services communautaires) za Amerika

  • Soma - Huduma za mahali unakaa (services communautaires) za Amerika
    Soma
  • Kusikiya - Huduma za mahali unakaa (services communautaires) za Amerika
    Kusikiya

Huduma za jamii ni huduma, musaada, vitu, na vipato vinavyo patikana kwa watu katika sherika zao. Kazi izi zinaweza tolewa bure ao kwamalipo ndongo na serkali, shirika za pamoja na shirika za dini zina saidiya serkali.

Msaada waki serkali

Mashirika ya huduma za kijamii ya serikali zinatowa msaada kwa watu wa jamii. Inasaidiya watu wanao kuwa na haja binafsi, kama vile familia inayo kuwa na mushahara mudogo, wanao kosa makao, na watu wanao ishi na ulemavu. Mpango wa serkali unakuwa ma muda ambao umewekewa mpaka na muelekezo kwa wauzuriyaji.

Hizi ni mipango wa serkali kwaku saidiya wakimbizi:

Mpango ya msaada waki pesa

Kwa watu walio na shida za kupata kazi, mipango miwili yana towa msaada waki pesa kwa muda mfupi: Msaada kwa muda kwa itaji za familia (TANF) kwa wazazi wanao Kuwa na watoto na msaada waki pesa kwa wakimbizi (RCA) kwa wale hawaja olewa na wakimbizi ambao wameolewa na hawana watoto.

Mpango wa msaada wa ziada kwa malisho (SNAP)

Mpango huu wa jimbo una towa msaada kwa watu wenye mshahara mdogo Marekani ili wanunue chakula. Mtu aliye katika mpango huu hupewa kadi inayo mu ruhusu kununua kiwango fulani cha chakula kila mwezi. Wakimbizi wanaweza kuomba msaada wa chakula katika ofisi za serikali za jimbo. Kiwango cha msaada ni tofauti katika kila muji na kufwatana na ukubwa na mapato ya familia

Usalama wa Ziada (SSI)

Hii ni mpango wa jimbo ya msaada waki pesa kwa watu ambao ni walemavu na wa zaidi ya miaka 65 na wanao kuwa na pato ndogo.

Mpango wa msaada kwa watoto

Jamii mojamoja hutowa kwa bure ao kwa malipo kidogo kazi zaku chunga watoto kwa watu wenye pato ndogo ili wapate ku tumika ao ku tafuta kazi.

Huduma za umma

Kila jamii ina kazi za uma zinazo patikana na kila mtu katika jamii. Zifuatazo ni chache ya zile huduma za umma za kawaida:

Za zarura na 911

Jamii zote zina idara za moto na kazi za zarura za matibabu. Kwaku pata msaada wa dharura, piga 911 kwa simu na umwambie msaidizi unachokihitaji (“polisi”, “Moto”, au “ambilensi”) na eneo lako. Ikiwa hauwezi eleza shida yako kwa kingereza, sema tu, “Msaada” au “Dharura”na usifunge simu. Mtandao wa simu ulio wazi utasaidia msaidizi kujua uliko.

Polisi

Maa ofisa wa polisi ni watumishi wa umma ambao wana linda umma na kusaidia watu. Ikiwa ofisa wa polisi anakujia na kukuomba usimame, fanya hivyo. Kila mara timiza ombi la ofisa na uwe mpole na mwenye heshima. Ikiwa hauwezi wasiliana na polisi, omba mtafsiri na ungoje kwa utulivu. Ikiwa unaweza, wasiliana na Agence de Réinstallation kwa usaidizi.

Vyumba vya vitabu

Vyumba vya vitabu vya umma zina vitabu na vifaa vingine, kama vile CDs na DVDs, ambayo wakahaji wanaweza azima bila malipo. Una lazimishwa kuomba kadi ya vyumba vya vitabu ili kuchukua vifaa toka hiyo. Chumba cha vitabu mara nyingi inatoa kwa watoto mipango za kusoma na mafunzo kama vile mazoezi ya mazungumzo kwa kingereza na mara nyingi wanakuwa na kompyuta za matumizi ya umma.

Pango na mapumziko

Pango za jimbo zinakuwa na uwanja wa matembezi na viwanja vya michezo kwa umma. Pango nyingi kuwa na kanuni kuhusu nini wageni wana pasha na hawapashwe ku fanya. Pango nyingi za jimbo ni bure, lakini pango zataifa zina weza lipisha pesa za kuhorozeshwa.

Msaada usio kuwa waki serikali

Shirika fulani za huduma zinaji shugulisha na mikopo kutoka kwa raia binafsi au na jumla ya mikopo na pesa za serikali. Wanakuwa na kundi ya waongozi wanao simamiya kazi yao na wanatakiwa ku towa ripoti ya umma kwa kila mwaka kuhusu kazi zao, lakini zina tenganishwa na serkali.

Aina hizi zote za shirika kwa ujumla zina kuwa chini ya moja ya ayo makundi matatu ya fwatayo:

Mashirika isiyo ya Kiserikali (NGOs)

Mashirika isiyo ya Kiserikali zina towa kazi kwa eneo zote nchini, kwa kawaida iliyo andaliwa na ofisi ya makao makuu katika muji mkubwa. Zimoja zina weza kutowa hizo msaada kwa wakimbizi. Kiasi, gharama na aina za kazi hizi pishana kutoka mahali kwa mahali, lakini wengi wanatowa zifwatayo:

Ushauri
Msaada wa hali yaku hama
Madarasa ya Kiingereza
Huduma za ajira
Huduma za utafsiri

Shirika za jamii (CBOs)

Hizo shirika zina tumika katika jamii za mahali na ina towa msaada wa mapumziko, jamii, na huduma za elimu kwa wanawanakaji wa jamii. Aina moja ya Shirika za jamii ambayo una weza kutana katika shirika lako ni shirika la msingi wa kabila (ECBO). ECBOs zime unduwa na wakimbizi wa zamani na wahamaji na zina saidiya wageni katika shirika zao. Zimoja zina towa darasa za elimu kwa watu wazima, zina andaa kundi za wa mama, na kushikilia kazi zaki mila na za mapumziko.

Shirika za imani (FBOs)

Shirika za imani zina jumlisha makanisa, miskiti, masinagogi na mahali zingine za maabudu ambazo lengo yayo niku kuza imani yao. Hata hivyo, kuna piya aina nyingi za shirika za imani, ambazo zina weza pokeya pesa au ku zinaweza ku tiwa kwa mawasiliyano na shirika nyingi za ki dini, ila lengo lao niku towa huduma kwa watu binafsi na familia zinazohitaji msaada bila kufwatana na dini yao. Wamoja wanakuwa na darasa za luga ya kingereza kwa watu wazima na wengine wana pana nguo za samani ambazo zimeisha tumikishwa.

⇠ Kila kitu kuhusu kufundishwa tabiya za Inchi (Orientation Culturelle)